………………
Na Sixmund Begashe, Dodoma
Club ya Michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT SPORTS CLUB) imejipanga vyema kukabiliana vikali na timu yeyote itakazo cheza nayo ili kuibuka na ushindi
mnono katika michezo ya Mei Mosi 2026 inayotarajiwa kufanyika Mkoani Njombe
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Club hiyo Bw. Elia Mutalemwa, Jijini Dodoma walipo kuwa wakiondoka kuelekea Mkoani Njombe kushiriki Mashindano hayo.
Bw. Mutalemwa amesema kuwa, maandalizi na mazoezi mazito waliyoifanya wachezaji wa Club hiyo ni dhahiri kuwa watarudi na ushindi wa kishindo.
Aidha Bw. Mutalemwa ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao hiyo kama walivyofanya wakazi wa Singida katika mashindano kama hayo mwaka 2025.
“Hatutakuwa na huruma na timu yeyote tutakayokutana nayo, itakula kichapo cha jangili, kwa kuwa tumejipanga kushinda michezo yote”. Alisema Bw. Mutalemwa
Ameushukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuiunga mkono kikamilifu Club hiyo katika hatua zote za maandalizi hadi kushiriki kwenye mashindano hayo hali inayoongeza morali zaidi kwa wachezaji.
Mashindano hayo ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya Sikuku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ukutanisha Club za michezo kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za umma hapa nchini na kwa mwaka huu 2026 kitaifa yanatarajiwa kufanyika Mkoani Njombe.




