WANANCHI KATA YA VIZIWAZIWA WAIFAGILIA HUDUMA YA RITA NA CCM KIBAHA MJI

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Wananchi Kata ya Viziwaziwa wamepongeza kwa dhati juhudi zinazofanywa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka kwa kushirikiana na Ofisi ya vizazi na vifo katika suala la kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.

Wananchi hao wakimemo wana chama wa CCM katika kata hiyo wameyasema hayo wakati wa mwendelezo wa ziara ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha mjini yenye lengo la kuweza kuwashukuru kwa kuweza kukiamini chama na kuweza kuwachagua viongozi katika ngazi ya udiwani,Ubunge,pamoja na nafasi ya Urais.

Wakizungumza kwa nyakati wamesema kwamba wamefarijika sana kwa zoezi hilo ambalo kwa upande wao litakuwa ni mkombozi mkubwa kutokana na hapo awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto hiyo ya kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

“Tunashukuru sana kwa zoezi hili ambalo limeweza kuwa ni msaada mkubwa sana wa kuweza kupata vyeti vya kuzaliwa kwa bei nafuu na sisi atuna budi kumshukuru Mwenyekiti wa CCM Kibaha mji pamoja na Ofisi ya vizazi na vifo,”wamesema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amebainisha ameamua kufanya ziara yake ya kushukuru ambayo inakwenda sambamba na kutoa huduma ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi.

Nyamka amebainisha kwamba zoezi hilo litawahusisha wananchi wote wenye vifa na kwamba lengo lake kubwa ni kuwasaidia wananchi kuwa na vyeti vyao vya kuzaliwa ambavyo pia vitawasaidia kwa kiasi kikubwa katika mambo yao mbali mbali.

Kwa upande wake Msajili kutoka Ofisi ya vizazi na vifo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha John Chuwa amesema kwamba hadi sasa wameshatoa huduma katika kata nne za Mbwawa,Visiga,Misugusugu pamoja na Viziwaziwa.

Ziara ya kushukuru ya Mwenyekiti wa chama cba mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka pia imewatembelea mabalozi wa mashina pamoja na kufanya mkutano wa hadhara uliowajumuisha wananchi na wanachama wa CCM.