MEELA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA SWALA LA WIZI.
MOSHI. Wimbi la wizi, hasa wa mita za maji, limeendelea kuwa changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, hali inayozua wasiwasi kwa wananchi na viongozi wa jamii. Kutokana na hali hiyo, viongozi wa dini wametakiwa kutumia nafasi zao kuzungumzia na kukemea vitendo hivyo pamoja na kuwaombea vijana wanaojihusisha na uhalifu…