Mvua ilivyoua watano, kukata mawasiliano
Mikoani. Mvua zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya mikoa nchini, zimesababisha vifo vya watu watano, uharibifu wa miundombinu ya majengo, barabara pamoja na kuathiri mazao. Pia, zimesababisha upotevu wa muda kwa wananchi, wanafunzi kukosa masomo na kupanda kwa gharama za usafiri katika maeneo mbalimbali yanayoendelea kukumbwa na mvua hizo. Mkoani Dodoma, mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia…