Serikali yaonya watakaoficha mafuta kusubiri yapande bei
Dodoma. Serikali imesema haitawavumilia wafanyabiashara wa mafuta ya vyombo vya moto ikiwamo petroli, watakaotumia mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati, kuficha bidhaa hiyo wakisubiri ipande bei, ikisisitiza vitendo hivyo vinahatarisha upatikanaji wa nishati kwa wananchi. Sambamba na hilo, imeagiza kuundwa kwa kamati maalumu ya kufuatilia mwenendo wa uingizaji wa mafuta nchini, kuhakikisha yanafika kwa wakati kwa…