RAIS DKT. MWINYI AIHIMIZA BENKI YA KCB KUSHIRIKIANA NA SMZ KUWAWEZESHA VIJANA
……. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akizungumzia changamoto zinazowakabili vijana, ameisisitiza benki ya KCB Tanzania kupitia programu ya kurudisha fadhila kwa jamii kushirikiana na Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji kutafuta njia bora na endelevu zitakazowanufaisha vijana, hususan katika suala la uwezeshaji wa mikopo kwa vijana…