Vibanda 72 vyafungwa Mbozi, wafanyabiashara wagoma
Songwe. Jumla ya vibanda 72 vinavyozunguka Soko la Ichenjezya, wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe, vimefungwa na maofisa mapato wa halmashauri kufuatia mgogoro wa malimbikizo ya kodi ya pango. Hatua hiyo imeelezwa kuchochewa na madai ya kutolipwa kwa kodi tangu mwaka 2021 katika vibanda hivyo. Kufungwa kwa vibanda hivyo kumesababisha wafanyabiashara 167 wanaofanyia biashara ndani ya…