WAZIRI WA FEDHA AZIKABIDHI TUZO ZA UBUNIFU ZA TRA
::::::: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa Tuzo za ubunifu kwa washindi 9 waliotoa mawazo bora zaidi yatakayosaidia kuendelea kuboresha huduma za kodi na kuongeza wigo wa kodi. Akikabidhi tuzo hizo, vyeti pamoja na hundi kwa washindi hao Februari 25.2026, Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar ameipongeza TRA kwa kuja na Tuzo hizo…