Sare ya Simba yalinda rekodi ya Yanga
Simba juzi Alhamisi, Machi 19, 2026 ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Pamba Jiji katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Matokeo hayo yameifanya Simba ipande hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointi 28 huku Pamba jiji ikibaki katika nafasi ya tano ikifikisha pointi 25….