Tamu, chungu ya bei maandalizi ya Eid, Bakwata yatoa ujumbe kwa waumini
Dar es Salaam. Wakati Waislamu nchini wakijiandaa kusherehekea sikukuu ya Eid kati ya kesho Ijumaa au Jumamosi, Machi 21, 2026, mfumko wa bei kwenye vyakula na nguo za watoto umekuwa kikwazo katika shamrashamra hizo, baadhi wakilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa hizo muhimu. Wamesema hali hiyo imewalazimu wengi kubana matumizi na wengine kubadili mipango yao…