Miili watumishi wa afya waliofariki kwa ajali ya boti Kigoma, yaagwa
Kigoma. Wananchi, watumishi na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kigoma wameaga miili ya watu saba waliokufa kwenye ajali ya boti. Huku wananchi wakisisitizwa kufuatilia taarifa ya hali ya hewa. Miili iliyoagwa ni ya watumishi wanne wakiwamo muuguzi msaidizi, Paul Luvanda (29), tabibu wa afya, Rachel Msalila (28), tabibu wa kinywa na meno, Joyce Kandole (29)…