ZAIDI YA BILIONI 8 ZATUMIKA KUBORESHA MTANDAO WA BARABARA WILAYANI ARUMERU

📌Wanawake na Vijana  wajengewa uwezo ushirikishwaji wa vikundi  📌Barabara ya Zege yawa Mkombozi kwa wakazi wa Machumba-Nkoarua Arumeru Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) imeendelea kuboresha na kukamilisha ujenzi wa barabara mbalimbali katika Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha, hatua inayolenga kurahisisha usafiri na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi….

Read More

RAIS MWINYI AJUMUIKA NA VIONGOZI,FAMILIA NA WANANCHI KATIKA MAZISHI YA NDUGU HAMZA KHAMIS

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafamilia pamoja na wananchi katika mazishi ya Ndugu Hamza Khamis Hamza, aliyefariki jana. Marehemu Hamza Khamis Hamza (75) amefariki jana alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Lumumba, Mkoa wa Mjini Magharibi. Mazishi hayo…

Read More

Boti yapinduka Ziwa Tanganyika, watumishi sita wa afya wafa maji

Kigoma. Watumishi sita wa Idara ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, mkoani Kigoma wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika Ziwa Tanganyika. Watumishi hao walikuwa wakitoka Kigoma Mjini kuelekea Kijiji cha Kagunga kutoa huduma ya chanjo walipokumbwa na ajali hiyo iliyosababishwa na upepo mkali uliosababisha mawimbi makubwa ziwani. Akizungumza katika eneo…

Read More

TMA yatoa tahadhari kwa watumiaji wa Ziwa Nyasa

Mbeya. Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imewataka wavuvi mwambao mwa Ziwa Nyasa kuchukua tahadhari kufuatia kuwepo kwa vipindi vya radi na upepo mkali wenye uwezo wa kusababisha ajali au kupinduka vyombo vya uvuvi majini. Mbali na wavuvi pia imewataka wananchi waishio mabondeni kuchukua tahadhari kubwa kufuatia udongo kufyonza…

Read More

WAHARIRI WATEMBELEA MRADI WA REA USAMBAZAJI WA UMEME VITONGOJI SITA WILAYANI LUDEWA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limetembelea mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji sita vilivyopo ukanda wa Ziwa Nyasa wilayani Ludewa mkoani Njombe, mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kiasi cha fedha Sh. bilioni 3.1. Utekelezaji wa mradi huo ulianza kutekelezwa Julai 13, mwaka 2025 na unatarajiwa kukamilika Aprili…

Read More

REA YAANZA USAMBAZAJI WA MAJIKO BANIFU 8,424 KIGOMA

Wakala wa Nishati Vijijini imeanza utekelezaji wa mpango mkakati wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia ili kufikia lengo la zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania ifikapo mwaka 2034 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia nishati ambayo ni salama kwa mtumiaji na rafiki kwa mazingira. Akizungumza wakati wa ugawaji wa majiko katika Wilaya Kibondo…

Read More

WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN

Watanzania SABA waliokuwa nchini Iran wamewasili jijini Dar es Salaam Machi 13, 2026, kufuatia operesheni ya uokozi iliyoratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Watanzania hao wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8:40 usiku kwa kutumia Shirika la Ndege la Uturuki, wakitokea nchini Uturuki ambako walipokewa awali…

Read More