Abra alivyoipa kisogo ndoto ya ofisini akigeukia uendeshaji mitambo ya kilimo
Morogoro. Wakati dunia ikiendelea kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8, simulizi ya Abra Kingologo inaibua tafakuri mpya kuhusu maana halisi ya ujasiri, ndoto na thamani ya kazi. Akiwa na umri wa miaka 23 na mhitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Abra amechagua njia ambayo wengi hawakuitarajia ya kuweka pembeni vyeti…