Kihongosi aanza ziara Shinyanga, ataja mambo matatu
Shinyanga. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi ametaja mambo matatu atakayoyafanya katika ziara yake ya siku nne mkoani Shinyanga iliyoanza leo Jumatano, Machi 4, 2026. Mambo hayo ni uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo ambayo Serikali imepeleka fedha na jambo jingine ni kusikiliza changamoto za wananchi. …