Wakulima wa kahawa Mbinga, wapata tumaini jipya
Mbinga. Wakulima wa zao la kahawa katika Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, wameanza kushuhudia ongezeko la tija, ubora na bei ya zao hilo, hali inayochochea matumaini mapya ya kuinua uchumi wa kaya na vijiji kwa ujumla. Mathalani, msimu wa mwaka jana, bei ya kahawa ilipanda kutoka wastani wa Sh7,000 hadi zaidi ya Sh11,000 kwa kilo…