UCHAMBUZI WA MJEMA: Ziara za Mwigulu zinaonyesha ombwe kwa taasisi imara
Katika ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba inayoendelea mikoa mbalimbali, tunashuhudia akitatua na kuzipatia ufumbuzi papo kwa hapo, kero zinazowakabili watanzania lakini hili linathibitisha ombwe la taasisi imara. Ninasema hivyo kwa sababu kuna kero au changamoto zingine zingeweza kutatuliwa na wateule wengine wa Rais kama wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi…