Baba alivyojaribu kupangua ushahidi wa kumkata mwanae vipande na kuvitumbukiza chooni-3
Jana katika sehemu ya pili ya simulizi ya mauaji ya kikatili ya mtoto Timotheo Mhulila, ambaye aliuawa na kisha kukatwa vipande vipande na kutumbukizwa chooni, tuliona namna shahidi ambao ni askari polisi walivyoeleza namna mshitakiwa, Joseph Mhulila alivyokiri. Katika ushahidi huo, shahidi aliyeandika maelezo ya onyo ya mshitakiwa, alieleza kuwa Mhulila katika maelezo yake aliweka…