Aliyemuua baba yake ahukumiwa kunyongwa hadi kufa
Arusha. Mahakama Kuu, Masijala Ndogo ya Bukoba, imemhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa Victor Alex baada ya kumkuta na hatia ya kumuua baba yake mzazi, Alex Marcel, kwa kumkata kwa panga. Mauaji hayo yalitokea Aprili 29, 2024 katika Kitongoji cha Rwamashanga, Kijiji cha Ruzinga, wilayani Karagwe, mkoani Kagera. Hukumu hiyo ilitolewa Machi 18, 2026 na…