Bei ya kakao yaporomoka, wadau watafuta suluhisho
Mbeya. Wakati baadhi ya wakulima wilayani Kyela mkoani Mbeya wakitishia kukata na kung’oa miti ya kakao kutokana na anguko la bei, Chama Kikuu cha Ushirika Kyela (Kyecu) kimewataka kuwa wavumilivu huku kikitoa matumaini ya kurejea kwa bei nzuri ya zao hilo. Kwa takribani miaka miwili iliyopita, bei ya kakao ilikuwa ikifikia hadi Sh32,000 kwa kilo…