Kauli hii haitolewi na mwanamume wa kweli
Kuna kauli siku hizi imekuwa maarufu sana mitandaoni na hata kwenye vijiwe vya kahawa: “Natafuta mke mwenye kazi, anisaidie maisha.” Ukiisikia mara ya kwanza unaweza kudhani ni kauli ya maendeleo, usawa wa kijinsia na mipango ya kisasa ya ndoa. Lakini ukiichambua vizuri, unaweza kubaini kuna harufu fulani ya uvivu iliyojificha nyuma ya maneno hayo matamu….