Simba yapanda nafasi ya pili ikiichapa TRA United

Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo timu hiyo sasa imesogea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikifikisha pointi 31 ikiishusha Azam FC ambayo ina pointi 29 katika nafasi ya tatu. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Dimba la Major General Isamuhyo, Mbweni, Dar es…

Read More

Msimu huu namba za Yanga zinakataa, mtihani uko hapa!

NAMBA ambazo Yanga walizitengeneza msimu uliopita wa ligi 2024-2025, zinaonekana kuwakimbia msimu huu wa 2025-2026 na watatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kuzifikia  huku mambo yakionekana kutowaendea vizuri. Yanga ambao wamemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara wakiwa kileleni, jana walianza mzunguko wa pili kwa kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar…

Read More

Ligi Kuu Zanzibar kupigwa Bara

BODI ya Ligi Zanzibar (ZBL), inatarajia kufanya marekebisho ya kanuni za mashindano ili kuruhusu timu za Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) kutumia viwanja vya Bara kwa ajili ya mechi. Hatua hiyo inalenga kuongeza ushindani wa ligi hiyo na kutoa fursa kwa wachezaji wa Zanzibar kuonekana zaidi na kutambulika kwenye soka la Tanzania. Akizungumza na Mwanaspoti, Mtendaji…

Read More

Ushindani mkali NBC PL wafungua vita mpya ufungaji bora

MISIMU mitano ya Ligi Kuu Bara imekuwa ikitawaliwa na mastaa wakubwa kutoka nje ya nchi wakitwaa kiatu cha ufungaji bora mara tatu,  lakini kwa sasa inaonekana mambo yanaweza kubadilika na mzani ukawa sawa. Kwa sasa staa kutoka DR Congo, Fabrice Ngoy anayechezea Namungo ndiye kinara wa mabao akiwa ameshafunga manane, lakini bado takwimu zinaonyesha kuwa…

Read More

Majeraha yavuruga mipango ya Yanga kutetea ubingwa

UNA mabao ya Yanga yapo nje kutokana na mitambo ya mabao kupata majeraha na kupewa muda wa kupumzika ili kutibiwa irejee kwenye ufiti. Kukosekana kwao kumechambuliwa na watalamu jinsi inavyoleta athari hasi. Katika mechi 15 Yanga imeshinda 11, sare nne, inamiliki mabao 31, imefungwa mawili, ina pointi 37. Kati ya mabao hayo Prince Dube kafunga…

Read More

ZPL kuongezwa thamani kuitangaza Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema lengo la kuwekeza fedha nyingi kwenye sekta ya michezo ni kuhakikisha inakuwa msingi unaowezesha kukuza vipaji, kuongeza ushindani na kuifikisha Zanzibar katika viwango vya kimataifa. Hayo yalielezwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi wakati alipokutana na uongozi wa taasisi ya Tanzania Securities Limited, Ikulu mjini Zanzibar….

Read More

Ugumu Simba v TRA United uko hapa!

KUNA dakika 90 muhimu leo zitapigwa pale Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni Jijini Dar es Salaam, Simba itakaporejea nyumbani kupambana na TRA United, kwenye mchezo ambao utakuwa wa ushindani mkubwa kila timu ikiwa inahitaji pointi tatu za jasho. Huu utakuwa mchezo wa mwisho kwa timu hizo kabla ligi kuu haijasimama kwa wiki mbili kupisha…

Read More

Mzenji TMA FC afunguka dili la Yanga

KOCHA wa TMA FC, Mzanzibar Haji Ali Nuhu, amesema hadi sasa hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa kati yake na uongozi wa Yanga, kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu za vijana, akiungana na Mohamed Badru, aliyewahi kufanya naye kazi. Kocha, Badru ambaye kwa sasa anasimamia programu ya Yanga Soccer School, iliyozinduliwa rasmi tangu, Novemba 15,…

Read More

Mtibwa vs Yanga mtego uko hapa!

YANGA inarudi uwanjani leo ikiendelea na ziara ya mechi za ugenini itakapokutana na Mtibwa Sugar na timu zote mbili zitakuwa na akili moja tu ya kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri. Huu utakuwa mchezo wa mwisho kwa timu zote kabla ligi haijasimama kupisha michezo ya timu za Taifa na Taifa Stars itakwenda Rwanda kushiriki michuano…

Read More

Mkataba wa Nashoni, Simba upo hivi!

SIMBA imefanya umafia baada ya kumsajili kiungo wa Singida Black Stars, Kevin Nashon kwa mkataba wa miaka miwili zikiwa ni siku chache tangu walipogomewa saini yake. Simba kabla ya kufanya maamuzi ya kumsainisha mkataba wa awali wa miaka miwili Nashon, ilishafanya utafiti wa kujua amebakiza muda gani Singida Black Stars. Nashon alijiunga na Pamba 04/08/2025 …

Read More