Mtihani wa makipa wazawa | Mwanaspoti

KIPA wa Mashujaa FC, Patrick Munthali ndiye aliyekuwa kinara wa clean sheet akifikisha 12 kwa wazawa msimu uliopita Ligi Kuu Bara, ambapo amezungumzia ugumu wa kuifikia rekodi hiyo. Munthali amesema alipata na majeraha, hivyo katika mechi sita dhidi ya Singida Black Stars, Pamba Jiji, Simba, KMC na Tanzania Prisons ndizo alipata cleansheets moja anayomiliki msimu…

Read More

Asukile atoa matumaini mapya Prisons

PAMOJA na kukiri kuwa na matokeo yasiyoridhisha, Nahodha wa zamani wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amesema bado ni mapema kuikatia tamaa timu hiyo, huku akiwatwisha zigo wakongwe na mastaa wa kikosi hicho kukaza kukwepa aibu ya kushuka daraja. Asukile aliyeitumikia Prisons kwa takribani miaka 11 kisha kuvishwa gwanda la Magereza, kwa sasa anahudumu kwenye benchi…

Read More

JKT Tanzania yakomaa na mambo manne

KATIKA kipindi hiki kirefu ambacho JKT Tanzania haina mechi ya mashindano, kocha mkuu wa kikosi hicho, Ahmad Ally ameweka wazi mpango wao kuhakikisha hawatoki kwenye mstari. Katika mpango huo, kocha huyo ametaja mambo manne anayokomaa nayo kuwa ni uimara wa mwili, ubora wa kiufundi, mbinu na mifumo ya uchezaji, pamoja na utayari wa kisaikolojia. Akizungumza…

Read More

Nyota Coastal Union kimeeleweka | Mwanaspoti

STRAIKA wa Coastal Union, Abdulkarim Segeja, amesema licha ya kuanza vibaya msimu huu, lakini kwa sasa timu imeonesha mabadiliko na mechi zilizobaki mkakati wao ni kutopoteza pointi. Coastal Union iliyowahi kutwaa ubingwa mwaka 1988 wakati inaitwa Ligi Daraja la Kwanza kabla ya sasa kufahamika Ligi Kuu Bara, inakumbukwa pia kushuka daraja msimu wa 2015-2016 ikiwa…

Read More

TRA United v Yanga mechi za kimkakati

MSAKO wa pointi tatu kwa Yanga unaendelea leo huku ikiwa na wimbi kubwa la mastaa majeruhi ambapo wameongezeka wengine wanne na kufikia sita, baada Clement Mzize na Dickon Job kuwa nje. Yanga inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36, leo ni mgeni wa TRA United, mechi ikichezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid…

Read More

Daktari aeleza kitaalamu chanzo majeraha ya mastaa Yanga

KAMA wodi ya wagonjwa sasa huko Jangwani inaelekea kujaa kufuatia idadi ya majeruhi kuongezeka ikiwa ni siku chache tangu kutangazwa kuwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Dickson Job na Clement Mzize watakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki sita, huku mmoja wa madaktari bingwa akitaja sababu na suluhisho lake. Madaktari wa klabu hiyo wamethibitisha…

Read More

Ishu ya Simba, Sowah yafikia hapa!

MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Swedi Mkwabi amesema suala la Jonathan Sowah bado lipo katika kamati ya nidhamu ya klabu hiyo, hivyo uamuzi wake utatolewa kila kitu kitakapokuwa sawa. Mkwabi aliyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa za Sowah kujibu tuhuma zinazomkabili zilizofanya uongozi wa klabu kumsimamisha tangu timu ilipokuwa ikijiandaa na mechi…

Read More

Kocha Pamba afungua ‘code’ ya Simba

WAKATI Pamba Jiji ikijipanga kuipokea Simba SC, kocha wa kikosi hicho, Francis Baraza amesema kazi kubwa waliyonayo ni kuwashika wekundu hao pabaya. Mechi hiyo itakayochezwa Machi 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Baraza alisema eneo lenye nguvu zaidi kwa Simba ni kiungo, hivyo watadili nalo kuhakikisha wanapata ushindi kirahisi wakiwa nyumbani….

Read More

Kisa Mayele, Dube aingia anga za Wasauzi

UONGOZI wa Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini, umeanza kumfuatilia mshambuliaji nyota wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Mzimbabwe, Prince Dube, ambaye mkataba wake na kikosi hicho unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu. Taarifa kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa mabosi wa timu hiyo wanaangalia uwezekano wa kumpata mshambuliaji huyo, baada ya kupata ugumu…

Read More