Wafanyakazi 471 wa gati la mafuta Tanga walalamikia kutolipwa stahiki
Tanga. Wafanyakazi 471 wa kampuni moja katika mradi wa ujenzi wa gati la kupokelea mafuta baharini kwa ajili ya bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP), wamewasilisha malalamiko katika Kliniki ya Sheria jijini Tanga wakidai kutolipwa stahiki zao za kazi. Kliniki hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inafanyika katika viwanja vya Tangamano,…