Serikali kutoa Sh8.1 bilioni kurejesha vivuko, madaraja Serengeti
Serengeti. Serikali imesema itatoa Sh 8.1 bilioni kwa ajili ya kurejesha vivuko na madaraja saba yaliyoharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ambazo zimeharibu miundombinu hiyo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema hayo leo Jumapili Machi 8, 2026 akizungumza katika Kivuko cha Mto Banagi, kilichopo hifadhini humo baada…