Ninja aelezea uzoefu anaoupata Championship
BEKI wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ anayeichezea Transit Camp inayoshiriki Championship, alisema anajifunza vitu vingi kutoka ligi hiyo anayocheza kwa mara ya kwanza, huku akifichua huko zaidi nguvu inatumika sana. Ninja aliyezaliwa Zanzibar Januari 21, 1998 akiwa na umri wa miaka 27 hivi sasa, alisema ugumu wa Ligi ya Championship ni kwa zile…