Wazazi wanavyoweza kudhibiti WhatsApp za watoto wao

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha usalama wa watoto mitandaoni, Kampuni ya teknolojia ya Meta Platforms, inayomiliki programu ya WhatsApp, imetangaza kuanzisha mfumo mpya wa akaunti zinazodhibitiwa na wazazi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 13. Tangazo hilo lililotolewa Machi 11, 2026, linakuja wakati dunia ikishuhudia ongezeko la wasiwasi kuhusu athari za mitandao ya…

Read More

Mapya yaibuka matokeo ya urais Tanzania

Arusha. Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) imebaini kuwepo kwa upungufu katika Katiba ya Tanzania unaozuia kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais mahakamani, ikisema kifungu kinachokataza hatua hiyo kinakiuka haki za binadamu. Katika hukumu iliyotolewa leo Ijumaa, Machi 6, 2026, kwenye kesi ya Ado Shaibu na wengine dhidi ya Jamhuri…

Read More

Viongozi 70 CCM Moshi wasaini kumkataa kigogo mwenzao

Dar es Salaam. Msuguano ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro unaonekana kuingia katika hatua ngumu zaidi baada ya viongozi 70 kusaini barua ya kutokuwa na imani na kigogo wa chama hicho ngazi ya wilaya. Taarifa za uhakika zilizolifikia Mwananchi, zinaeleza miongoni mwa waliosaini barua hiyo iliyotumwa kwa Katibu wa…

Read More

Makubaliano Musongati yafungua ukurasa mpya uchimbaji Nikeli Afrika Mashariki

Dar es Salaam. Kampuni ya Lifezone Metals inayomiliki Tembo Nickel, imesaini makubaliano ya miezi 14 na Serikali ya Burundi kuhusu maendeleo ya mgodi wa Nikeli wa Musongati. Hatua hiyo inatajwa kuwa inaenda kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya madini na miundombinu. Akizungumza kuhusu makubaliano hayo yaliyosainiwa Machi 10, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa Tembo Nickel,…

Read More

Diarra anawapiku hapa Manula, Kassali

MAKIPA Djigui Diarra wa Yanga, Aishi Manula (Azam) na Mahamadou Tanja Djibrilla Kassali Djibo (Simba), wameendelea kuonyesha ubora katika mechi mbalimbali hasa za Ligi Kuu Bara, huku viwango vyao vikiwa ni msaada kwa timu zao. Kwa jumla makipa hawa wameokoa hatari 16 zilizodhaniwa zingewanyima cleansheet na kuwaacha waliojaribu kuwafunga wakishika vichwa kutokana na ufundi wao…

Read More

BAADA YA SADC KUITAJA TANZANIA KINARA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA; KAMISHNA LUOGA ATAKA WATUMISHI KUKUZA MATUMIZI YA NISHATI HIYO

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amewataka Watumishi wa Wizara ya Nishati kuendelea kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ili kufanikisha ajenda hiyo  ambayo kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ameeleza kuwa ajenda ya nishati safi ya kupikia tayari imeanza kuonesha mafanikio…

Read More

JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE HANDENI MJI KUZINDULIWA MACHI 5

  Na Mwandishi Wetu KATIKA kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Halmashauri ya Mji Handeni imejipanga kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwamo uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. Akizungumza kuhusu maandalizi ya maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maryam Ukwaju, amesema halmashauri hiyo inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wanawake katika…

Read More

Iran yaishambulia UAE, vita yazidi kupamba moto

Mashambulizi mapya yamezuka katika vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati baada ya Iran kushambulia Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) leo Jumanne, hatua inayotafsiriwa kama kulipiza kisasi dhidi ya Marekani na washirika wake. Mashambulizi hayo yanakuja wakati vita kati ya Iran na muungano wa Marekani na Israel ikiingia wiki ya tatu, huku zaidi ya watu 2,000…

Read More