Takukuru yawarejeshea wananchi Sh500,000 walizochangishwa kupata umeme
Mbeya. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mbeya (Takukuru), imewarejeshea wananchi 20 wa Mtaa wa Ilomba jijini humo Sh500,000 walizochangishwa na Alex Nyagawa kwa ajili ya kuwaunganishia huduma ya umeme majumbani. Inadaiwa kuwa, Nyagawa aliwashawishi wananchi hao wampatie fedha hizo ili awaunganishie huduma hiyo kwa bei nafuu inayotolewa na Wakala wa Nishati…