Mafwele, wengine 42 kutoa ushahidi kesi ya askari wanaodaiwa kughushi vibali vya silaha

Dar es Salaam. Mashahidi 43, akiwemo Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Faustine Mafwele, wanatarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya kughushi vibali vya kumiliki silaha inayowakabili watu tisa, wakiwemo maofisa sita wa Jeshi la Polisi. Wakili wa Serikali, Cathbert Mbiling’i, ameieleza Mahakama…

Read More

Sura tatu ziara ya Kihongosi Tabora, Kigoma

Ziara ya siku saba ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, katika mikoa ya Tabora na Kigoma, imeibua matumaini kwa wananchi, lakini baadhi ya watendaji wa Serikali walijikuta kwenye wakati mgumu mbele ya kiongozi huyo. Ugumu huo ulitokana namna ya Kihongosi alivyokuwa akiwabana akiwataka kutoa maelezo ya kina…

Read More

Chakwera awasili Tanzania, atumwa na Jumuiya ya Madola

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Malawi, Lazarus Chakwera amewasili nchini kwa ziara ya kikazi usiku wa kuamkia leo Alhamisi Aprili 9, 2026, ikiwa ni takriban miezi sita imepita tangu ilipotangazwa angewasili kama kiongozi wa ujumbe wa Jumuiya ya Madola. Novemba mwaka jana, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Shirley Botchwey, alimteua Chakwera kuwa mjumbe…

Read More

Mambo sita mwanao anayohitaji kuyasikia

Dodoma. Watoto wadogo ni watu kamili wenye hisia kama sisi watu wazima. Hata kama wakati mwingine hawawezi kusema wazi wazi, ukweli ni kwamba akili zao ni kama dodoki linalonyonya kimya kimya yale wanayoona tukiyasema na kuyatenda. Unaweza, kwa mfano, kusema jambo dogo kwa mtoto tena bila kumaanisha lakini jambo hilo likawa sumu itakayoharibu kabisa maisha…

Read More

Wasiwasi ulioibuka kuhusu kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Burundi kutoka Tanzania ‘kwa kutumia nguvu’ — Global Issues

Hadi kufikia mwishoni mwa Novemba 2025, kulikuwa na zaidi ya wakimbizi 140,000 wa Burundi katika nchi jirani ya Tanzania, ambao wamekimbia machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi nchini Burundi. Wakati maelfu wanaendelea “kurejeshwa kwa hiari”, afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) anasema maelfu bado wanaweza kuhitaji ulinzi wa…

Read More

Mke wa Kiongozi Mkuu wa Zamani wa Iran Auawa Nyumbani Kwake

Global Publishers March 2, 2026 0 Comments Kituo cha televisheni ya taifa ya Iran, Channel Two, kimethibitisha kuwa Mansoureh Khojasteh Bagherzadeh, mke wa Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran Ali Khamenei, ameuawa nyumbani kwake. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bagherzadeh aliuawa katika mazingira ambayo bado hayajawekwa wazi kwa kina na mamlaka za Iran. Awali, magazeti…

Read More

Sera ya vijana EAC yatia matumaini, sauti yao bado changamoto

Dar es Salaam. Wakati nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zikiendelea kuboresha sera ya vijana ya 2025–2030, wadau wamesema inaleta matumaini kwa maendeleo ya vijana, lakini bado kuna changamoto ya ushirikishwaji na utekelezaji. Hayo yameelezwa leo Machi 18, 2026 katika mkutano wa kikanda wa afya ulioandaliwa na Baraza la Wabunge Vijana wa Afrika…

Read More