Majonzi mwili wa Naomi ukipatikana katika mazingira tata
Iringa. Majonzi mazito yametanda katika familia moja mjini Iringa baada ya kupatikana kwa mwili wa Naomi Kivamba (13) aliyekuwa akisoma darasa la saba Shule ya Msingi Njiapanda aliripotiwa kupotea ghafla nyumbani kwao kabla ya kupatikana akiwa amefariki dunia. Ndani ya nyumba ya familia hiyo kulikuwa na hali ya huzuni iliyochanganyika na mshangao, huku watu wakikusanyika…