Familia yaiangukia Serikali kupotea kwa mtoto wao

Mbeya. Zikiwa zimepita siku 12 tangu kutoweka kwa mtoto Frank Aliko (10), familia yake imeiangukia Serikali ikiitaka kufanya uchunguzi wa kiintelenjia kufanikisha kupatikana kwake. Frank (10), mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ikulu iliyopo Kata ya Ilomba, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, inadaiwa ametoweka nyumbani tangu Machi 4, 2026 baada ya kupelekwa…

Read More

Saratani ya utumbo yashika kasi, visababishi vyatajwa

Dar es Salaam. Wataalamu wa afya nchini wamesema saratani ya utumbo mpana, kitaalamu ikiitwa Colorectal Cancer, imeanza kuongezeka kwa kasi nchini, huku mabadiliko ya mtindo wa maisha yakitajwa kuwa sababu kubwa inayochangia ongezeko hilo. Miji mikubwa imetajwa kuwa hatarini, huku wataalamu wakisema ongezeko hilo linachangiwa zaidi na mabadiliko ya mtindo wa maisha, ikiwamo ulaji wa…

Read More

Ewura yatangaza bei mpya ya mafuta, yapanda bandari zote

Dar es Salaam. Watumiaji wa bidhaa za mafuta Tanzania wataendelea kuugulia maumivu ya ongezeko la bei baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei kikomo zitakazotumika Machi mwaka huu. Katika bei hizo, watumiaji wa mafuta ya dizeli wameshuhudia ongezeko la bei zaidi ikilinganishwa na wale wa petroli na mafuta ya taa. Kwa…

Read More

Dickson Job nje miezi miwili Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, amethibitisha kwamba, nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Dickson Job, hatakuwa sehemu ya mechi ya kesho Alhamisi dhidi ya Singida Black Stars kufuatia kuumia enka. Kwa mujibu wa Pedro, Job aliyeumia enka katika Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba iliyomalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana wikiendi iliyopita, anatarajiwa kuwa nje…

Read More

FYATU MFYATUZI: Leo Fyatu navifyatua vitegemezi vya vigogo

Baada ya kushuhudia kilichotokea kaya jirani kwa fyatu mwenzangu hayati Ken Aliyeunda kaya, nimestuka na kuogopa japo najiamini sana. Kwa wasionyaka inshu ni kwamba, kule Dhambia, kitegemezi cha munene wa zamani kilijikuta pakanga. Katika kufanya uchunguzi na unoko, lisrikal la kule kwa ‘roho’ mbaya yake si liliinyaka kuwa kitegemezi cha munene wa zamani aliyenyotoka roho…

Read More

Mradi wa umeme jua Shinyanga waingizwa gridi ya taifa

Shinyanga. Awamu ya kwanza ya mradi wa umeme jua katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imekamilika kwa asilimia 95.5 ikiwa sehemu ya mpango wa kupunguza changamoto ya umeme katika mkoa huo na mingine ya Kanda ya Kiwa. Hayo yameelezwa na leo Machi 13, 2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Lazaro Twange…

Read More

WANAFUNZI WA MADRASA ,WAALIMU KUTOKA KONDOA WATHIBITISHA KWA MUNGU HAKUNA KUBWA NGORONGORO

Mwenyezi Mungu akitaka jambo litokee  hutokea ndivyo ilivyotokea, uumbwaji wa Kasoko ya Ngorongoro zaidi ya miaka milioni 2.5 iliyopita ambapo mlima mrefu uligeuzwa kuwa bonde la Ngorongoro. Wanafunzi wa madrasa kutoka jimbo la Kondoa mkoani Dodoma pamoja na walimu wao wameshuhudia uwezo huo wa Mwenyezi Mungu walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro katika ziara iliyoandaliwa na mbunge…

Read More