Umuhimu wa ujenzi wa imani katika jamii ya Kiislamu
Tatizo la jamii ya Kiislamu leo hii, si ukosefu wa mwonekano wa kidini au ukosefu wa misikiti, au udhaifu wa mawaidha. Minara ya misikiti na majukwaa ya kuhubiri yamekuwa mengi, tatizo lipo katika mwonekano wa nje wa Waislamu na kukosekana utekelezaji wa imani ya kweli. Watu wengi utawakuta wanatimiza ibada vizuri, lakini wanakosea katika utekelezaji…