Majembe saba yampa jeuri kigogo Simba, atuma salamu
LICHA ya Simba kutoka suluhu dhidi ya Yanga katika Dabi ya Karikoo wikiendi iliyopita, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Crescentius Magori, amesema usajili uliofanyika dirisha dogo umezaa timu mpya itakayofanya makubwa msimu huu, huku kocha wa zamani wa klabu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akiwataja mastaa watatu wakali. …