Haya hapa maeneo muhimu kukuza sekta ya fedha
Dar es Salaam. Serikali imeainisha maeneo nane ya kipaumbele ndani ya sekta ya fedha ambayo yakitumika ipasavyo kwa ushirikiano na sekta binafsi yanaweza kuharakisha ukuaji wa uchumi. Maeneo hayo ni pamoja na ufadhili wa tabianchi, mabadiliko ya tabianchi, huduma za kifedha za Kiislamu, udhibiti wa mali za kidijitali, upatikanaji wa mitaji kwa biashara changa na…