Sababu TPA kuja na ada mpya, kuziahirisha

Dar es Salaam. Siku moja baada ya ada mpya ya uendelezaji wa miundombinu ya bandari (PID) kulalamikiwa, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeeleza sababu za kuianzisha na kuisogeza hadi Julai mosi mwaka huu. Ada hizo mpya zilipaswa kuanza kutumia Machi 8, 2026 lakini baada ya kutangazwa na kuibua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau…

Read More

Mauzo ya Tanzania nje yaongezeka, wachumi wakitoa tahadhari

Dar es Salaam. Wataalamu wa uchumi wamesema huenda mauzo ya Tanzania katika masoko ya nje yakaathirika katika siku za usoni ikiwa uchumi wa nchi wanunuzi utasinyaa. Kusinyaa kwa uchumi wao kutapunguza uwezo wao wa kununua bidhaa za Tanzania, kushusha kiwango cha mahitaji au kubadili aina ya bidhaa wanazohitaji. Haya yanasemwa wakati ambao Tanzania imerekodi ongezeko…

Read More

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA VIJANA KATIKA KUMBUKIZI YA KUZALIWA BABA WA TAIFA HAYATI MWL. J.K NYERERE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa vijana kusimama imara na kulinda umoja, kujenga uadilifu, kutumia elimu na ubunifu katika kukuza maendeleo ya nchi ili kuweza kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua…

Read More

VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TIBA ASILI NA MAZINGIRA

 Na Mwandishi Wetu Katibu Mkuu wa TRAMEPRO, Boniventura Mwalongo, ametoa wito maalumu kwa vijana nchini, Afrika Mashariki na duniani kote kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya tiba asili na uhifadhi wa mazingira, akizitaja kuwa ni nguzo muhimu za ajira, uchumi na maendeleo endelevu. Akizungumza kupitia ujumbe wake maalumu kwa vijana, Mwalongo amesema dunia ya sasa…

Read More

Kichanga wa miezi tisa aokotwa jalalani Mbozi

Songwe. Wakazi wa Mtaa wa Msaki, Kata ya Ichenjezya, wilayani Mbozi mkoani Songwe, wamekumbwa na taharuki baada ya mwili wa mtoto mchanga wa kike, anayekadiriwa kuwa na miezi tisa, kupatikana ukiwa ndani ya bahasha na kutupwa kwenye dampo la takataka lililopo mtaani hapo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)…

Read More

Dkt. Mwigulu: Wanafunzi Bora Kusomeshwa Nje Kupitia Samia Scholarship

Global Publishers March 10, 2026 0 Comments WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba. WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema wanafunzi watakaofaulu kwa viwango vya juu watanufaika na ufadhili wa masomo kupitia mpango wa Samia Scholarship unaotolewa na Serikali. Dkt. Mwigulu amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi katika ziara yake mkoani Rukwa, ambapo pia aliwasilisha salamu maalum…

Read More

Samia atunukiwa shahada ya saba ya heshima

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameongeza orodha ya heshima anazopata kimataifa baada ya kutunukiwa shahada ya saba ya heshima, safari hii kutoka Chuo Kikuu cha Nasarawa nchini Nigeria. Shahada hiyo ya heshima imetolewa na chuo hicho kikuu leo, Jumamosi, Aprili 11, 2026, kwa kutambua mchango wa Rais Samia katika kuimarisha uongozi…

Read More

Wazazi wapewa somo kulea vipaji vya watoto nje ya darasa

Dar es Salaam. Ili kuwafanya watoto wajiamini, wawe wadadisi wa mambo pamoja na kuwaandalia mazingira bora ya ajira baadaye, wazazi na walezi wametakiwa kuwekeza katika ujuzi mbalimbali walionao watoto hao. Watoto wakiendelezwa kwenye maeneo kama sanaa ya muziki au michezo, watajenga kesho iliyo bora sambamba na kuwawekea msingi mzuri wanapokuwa darasani. Akitoa rai hiyo Aprili…

Read More

Maswa waomba kupatiwa elimu ya lishe, kupunguza udumavu

Maswa. Wananchi wilayani Maswa mkoani Simiyu wameiomba Serikali kuongeza juhudi za utoaji wa elimu ya lishe katika ngazi ya jamii, ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto ambalo bado linaendelea kuathiri familia nyingi. Wakizungumza Aprili 8, 2026, baadhi ya wananchi wamesema kuwa licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali na wadau wa afya, bado uelewa…

Read More