Wazawa wajitosa kuendesha taksi mtandao baada ya Uber kuondoka
Dar es Salaam. Ikiwa ni takribani miezi miwili sasa tangu kampuni ya kimataifa ya taksi mtandao ya Uber kufunga shughuli zake nchini, wazawa wameibuka na jukwaa kama hilo wakisema muundo wake umezingatia matakwa na mahitaji ya Watanzania. Jukwaa jipya la Izze limetambulishwa sokoni jana Machi 18, 2026 na linatarajiwa kuongeza ushindani katika soko la Tanzania…