DPP awaongezea mashtaka hadi 32 maofisa wa polisi wanaodaiwa kughushi vibali vya silaha
Dar es Salaam. Jamhuri imefanya mabadiliko katika hati ya mashtaka kwenye kesi ya kughushi vibali/leseni za kumiliki silaha, kwa kuongeza mashtaka 16 mapya, yakiwemo ya kukutwa na mihuri ya kughushi ya Jeshi la Polisi Tanzania. Kesi hiyo inawakabili watu tisa, akiwemo maofisa sita wa jeshi hilo. Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkaguzi wa Polisi mwenye…