Na Byera Deus ,Bukoba
MBUNGE wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhandisi Johnston Mtasingwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Dini wameungana na wananchi wa Kata ya Kibeta katika mtaa wa Anyama kushiriki Ibada ya kuaga miili ya watoto wawili kati ya Wanne wa familia mbili waliofariki kutokana na Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Aprili 17,2026 katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, ambayo ilisababisha vifo vya watoto wanne
Majina ya watoto waliofariki ni Eliza Edmund(13), mwanafunzi wa shule ya msingi Kashabo,Darasa la sita,Edwini Edmund(10), mwanafunzi wa darasa la nne Kashabo, Munihadi Mickidadi(13) aliyekuwa anasoma darasa la nne shule ya msingi Pamoja na Jamia Mickidad(5).
Akizungumza wakati wa kuaga miili ya watoto hao Mhandisi Mtasingwa ambaye ni Mbunge wa Bukoba Mjini amesema licha ya kuwa na majukumu ya vikao vya Bunge alipata taarifa saa 12 asubuhi.
Ambapo alituma msaada wa awali na mara baada ya kuuliza swali lake Bungeni alianza safari ya kurudi jimboni na alifika saa 6 usiku kuungana na familia hizo.
Amesema amesikitishwa na vifo vya watoto hao ambapo ametoa ombi kwa TANROAD na TARURA kuzibua mitaro hasa kipindi hiki cha mvua huku akiwataka wananchi kukagua nyumba zao mara kwa mara katika msimu huu wa mvua
Ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa wananchi waliopoteza mifungo na makazi na kuomba waendelee kuchukua tahadhari kwani mvua Bado ni nyingi na nitaendelea kunyesha na kuomba wananchi kuendelea kushirikiana pale matatizo yanapojitokeza
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima watoto wengine wawili ambao wamefariki katika tukio hilo tayari wamezikwa kata ya Maruku Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
“Nimesikitishwa kuwa na vifo hivyo ambavyo vimekatiza ndoto za watoto wadogo ambao walikuwa na malengo makubwa ya badae.Mvua hizo ambazo zimenyesha baadhi ya wanchi wamepoteza mifungo yao hasa kuku wengi wamesombwa.
“Wengine wamepoteza makazi hivyo nitoe mwito kwa wananchi wanaoishi mabondeni na kando kando ya Ziwa Victoria kuchukua tahadhari kabla ya vifo havijaongezeka.”
Ibada ya kuaga miili hiyo imeongozwa na Mchungaji Ediso Rugemeleza Mchungaji wa Usharika wa kanisaa kuu La Kiinjili la Kilutheri KKKT Dayosisi Kasikazini Magaribi
Ambapo ametumia fursa hiyo kwa kuzishukuru taasisi za serikali kufanya uokozi na wananchi Kujitolea ambao anadai kuwa hiyo ndio misingi ya utu. Vifo hivyo vimetokea baada ya ukuta wa hotel ya Perfect kuzidiwa na maji na kuangukia nyumba za majirani na kusababisha vifo vya watoto hao.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
