Man City Yaifunga Arsenal 2-1, Mbio za Ubingwa Zapata Moto Mpya

Global Publishers
April 19, 2026
0 Comments

Erling Haaland ameibuka shujaa wa Manchester City baada ya kufunga bao la ushindi lililoihakikishia timu yake ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal FC, matokeo yaliyotikisa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

City walianza kwa kasi na kupata bao la kwanza kupitia Rayan Cherki, aliyefunga bao la kuvutia baada ya kupita mabeki kadhaa kwa ustadi mkubwa. Bao hilo lilionekana kuwapa wenyeji udhibiti wa mchezo mapema.

Hata hivyo, makosa makubwa ya kipa Gianluigi Donnarumma yaliwapa Arsenal nafasi ya kurejea mchezoni, baada ya kumpa zawadi Kai Havertz aliyesawazisha kwa urahisi kufuatia uzembe huo.

Licha ya kusawazishwa, City hawakukata tamaa. Waliongeza presha hadi pale Haaland alipofunga bao la ushindi, akionyesha kwa mara nyingine ubora wake katika mechi kubwa.

Ushindi huo unaipa Manchester City nguvu kubwa katika mbio za ubingwa, huku ukipunguza zaidi pengo la alama dhidi ya Arsenal na kuongeza presha kwa vinara hao wa ligi.

Kwa upande wa Arsenal, matokeo hayo ni pigo kubwa, hasa baada ya kupoteza uongozi waliokuwa nao hapo awali, hali inayofanya mbio za ubingwa kuwa wazi zaidi huku msimu ukiingia hatua za mwisho.

Wiki mbili zilizopita, tofauti ya pointi ilikuwa tisa. Sasa ni tatu tu. Na zaidi ya hapo, City bado wana mchezo mkononi.