………..
Na. Sixmund Begashe, Njombe
Timu ya mpira wa Pete ya Club ya Michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeiadhibu vikali Timu ya Pete ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mabao 46-6 katika michuano ya Michezo ya Mei Mosi inayoendekea Mkoani Njombe.
Katika mchezo uliochezwa katika hali ya ukungu na mvua za rasha rasha, wachezaji wa timu ya Maliasili walionekana wakicheza kwa kasi ya ajabu na kuzitumia vyema nafasi walizopata hali iliyopelekea kuwashinda wapinzani wao kwa utitiri wa magoli.
Akizungumzia ushiriki wa Wizara katika mashindano hayo, Kaimu Mratibu wa Dawati la Michezo Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. George Rwezaura amesema pamoja na kujenga mshikamano, udugu na umoja wa Kitaifa, pia wanalengo la kutangaza shughuli za Wizara na Taasisi zake hasa kupitia ushindi katika michezo yao.
“Pamoja na Mpira wa Pete, leo timu yetu ya wanawake mchezo wa Kamba imeiburaza vibaya timu ya TPDC 2-0 na Mpira wa Miguu timu yetu imeshibana nguvu na timu ya Ulinzi huku sisi tukiongozo kundi tulilopangiwa”. Bw. Rwezaura
Wakizungumzi mchezo wa Kamba kati ya Maliasili na TPDC wanawake, Bw. Yohana Ngalupela, Mkazi wa Makete amesema michuano ni mikali lakini timu ya Maliasili ikionesha ubabe dhidi ya timu zingine.
“Hawa wanaonekama wamejipanga sana, sijuitii kuishangilia maana inatuheshimisha wakazi wa Njombe kwa kuwa niwahifadhi wenzetu”. Aliongeza Bw. Ngalupela.



