……….
Na: MWANDISHI WETU, CHAMWINO
Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amewapongeza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri kwa utendajikazi wao uliofanikisha utekelezaji wa miradi mingi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini.
Dk. Mwigulu ametoa pongezi hizo Aprili 19, 2026, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa maji wa miji 28, tukio lililofanyika wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
“Nikupongeze Mhe. Aweso na Katibu Mkuu mnafanya kazi nzuri sana, mmefuta visima hewa na miradi hewa,” amesema Dk. Mwigulu.
Katika hatua nyingine, Aweso amesema mradi huo ni muhimu na Wizara ya Maji itasimamia kikamilifu usambazaji wa maji kwa wananchi ili vijiji 1,575 vilivyobaki nchi nzima viweze kupata maji safi, salama na yenye kutosheleza.
Mradi wa maji wa miji 28 ni mradi kabambe nchini wenye lengo la kuongeza mtandao wa usambazaji maji nchini ili kuwawezesha wananchi wa maeneo mbalimbali kupata maji kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

