Pipijojo Aachia Video ya “Siachiki” Kazi Yake Ya Kwanza Chini ya Nandy

Global Publishers
April 14, 2026
0 Comments

Msanii Pipijojo ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa “Siachiki”, ikiwa ni kazi yake ya kwanza tangu kujiunga na lebo ya The African Princess inayomilikiwa na mwimbaji Faustina Mfinanga maarufu Nandy.

Wimbo huo umebeba ujumbe wa uthabiti, kujituma na msimamo wa kuendelea kushikilia unachokiamini bila kuyumbishwa na changamoto. Kupitia “Siachiki,” Pipijojo anaonesha mabadiliko ya kisanii na kuingia katika hatua mpya ya kitaaluma.

Siachiki” unamwonesha Pipijojo akijitambulisha upya chini ya lebo mpya, huku akilenga kuimarisha nafasi yake kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.