MIRADI YA BILIONI 19.2 YAPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2026 WILAYA YA UBUNGO

………….

Mwenge wa Uhuru 2026 unaendelea kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo April 16, 2026 katika Wilaya  ya Ubungo miradi ya maendeleo 7 yenye thamani  19,214,407,774.81 imepitishwa na Mwenge wa Uhuru hakuna mradi uliokataliwa.

Aidha katika miradi hiyo Mwenge wa Uhuru  umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali  ya maendeleo ikiwemo mradi wa kikundi cha vijana Malumalu Kata ya Msigani, ujenzi wa Maktaba na Ukumbi Shule ya Sekondari Barbro Johnson, na ujenzi wa barabara ya Hondogo Shija kata ya Kibamba, 

Vilevile miradi mingine ni ujenzi wa  zahanati Msakuzi, mradi wa maji mbezi msumi, ujenzi wa shule mpya ya sekondari Muungano Goba, na mradi wa Nishati safi kampuni ya Moto safi.

Mwenge wa Uhuru 2026 leo April 17, 2026 unaendelea Wilaya Kinondoni ambapo utakagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo