EPL Kwa Moto leo, Nani Kuvuna Alama Tatu, Liverpool Kukiwasha na Everton

Uwanja wa Hill Dickinson, Liverpool Leo tarehe 19 kuanzia saa 16:00 kwa muda wa Afrika Mashariki uwanja mpya wa kifahari wa Hill Dickinson utashuhudiwa moja ya mechi zenye historia kubwa katika soka la Uingereza, ambapo Everton watakuwa wenyeji wa Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Uwanja huu mpya wa Everton uliopo kwenye eneo la kivutio cha mbele ya maji (waterfront) unatarajiwa kuwa umejaa mashabiki zaidi ya 52,000, hali itakayowapa motisha zaidi wachezaji wa Everton kwa kuwa huu ni mchezo wao wa kwanza wa derby kwenye uwanja huu mpya baada ya kuondoka Goodison Park .

Liverpool wanaingia uwanjani wakiwa na uwezekano wa kushinda, mbele ya Everton. Hata hivyo, Everton wana rekodi nzuri wanapocheza nyumbani kwenye mechi kubwa, kwani hawajapoteza katika mechi 7 kati ya 9 zilizopita wakiwa wenyeji, wakishinda mechi 2, sare 4 na kushindwa mara 3 tu .

Kwa upande wa nafasi kwenye msimamo, Liverpool wana pointi 52 wakiwa nafasi ya 5, wakati Everton wana pointi 47 wakiwa nafasi ya 8, hivyo ushindi kwa timu yoyote utakuwa na athari kubwa katika kinyang’anyiro cha kufuzu kwa michuano ya Ulaya (UEFA Champions League na Europa League) kwani kuna tofauti ya pointi 5 pekee kati ya nafasi ya 4 hadi 9 .

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, Everton wamekuwa na kasi nzuri nyumbani msimu huu wakiwa wameshinda mechi 6 kati ya 16, sare 4 na kushindwa 6, wakiwa wamefunga mabao 21 na kufungwa 19,

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Huku Liverpool wakiwa na rekodi ya ugenini ya ushindi 6, sare 3 na kupoteza 7 kati ya mechi 16, wakiwa wamefunga mabao 23 na kufungwa 25 . Katika mechi 10 za mwisho za derby, Liverpool wameshinda mara 6, Everton mara 2, huku sare zikiwa 2, na jumla ya mabao ni 15 kwa Liverpool dhidi ya 8 kwa Everton. Mechi ya mwisho kati ya timu hizi ilipigwa Septemba 20, 2025 kwenye uwanja wa Anfield na Liverpool walishinda 2-1.

Kocha wa Everton, David Moyes, anatarajiwa kusimama Beto mbele akiungwa mkono na Iliman Ndiaye na Kiernan Dewsbury-Hall, huku nyuma wakiwemo James Tarkowski na Jarrad Branthwaite ambao wameweka clean sheet mara 2 kwenye mechi 5 zilizopita .

Kwa upande wa Liverpool, kocha Arne Slot anakosa nyota wake wa pembeni, Conor Bradley na Joe Gomez kwenye safu ya ulinzi kutokana na majeraha, Mohamed Salah, ambaye amekuwa akifunga katika mechi 3 za mwisho dhidi ya Everton, anatarajiwa kuwa tishio kubwa kwa ulinzi wa Everton.

Mabingwa wakutoa Odds kubwa, wamesha zitoa Tandika jamvi lako upate maokoto

Kumekuwa na Wasiwasi juu ya uwezo wa Liverpool kushinda mechi hii kutokana na kasi nzuri ya Everton chini ya David Moyes, hasa baada ya kufunga mabao 3 dhidi ya Chelsea na 3 dhidi ya Newcastle katika mechi za hivi karibuni . Mchezo huu unaahidi kuwa na mivutano mikubwa kwa kuwa ni derby na una athari ya moja kwa moja kwenye nafasi za kufuzu michuano ya Ulaya kwa Liverpool