© UNICEF/Oleksii Filippov
Mwanamke kijana amesimama kati ya viti vilivyovunjwa vya uwanja wa michezo huko Kharkiv, kaskazini-mashariki mwa Ukrainia.
Baraza la Usalama lakutana katika kikao cha dharura saa tatu usiku kushughulikia mzozo unaozidi kuongezeka nchini Ukraine. Mkutano huo wa wazi unafuatia ombi rasmi kutoka kwa Kyiv likitaja kuongezeka kwa mashambulizi ya anga ya Urusi, ikiwa ni pamoja na mashambulizi mabaya katika jiji la Dnipro. Ukraine imeripoti kuwa kati ya mwishoni mwa mwezi Machi na katikati ya Aprili, zaidi ya ndege zisizo na rubani 5,000 na makombora zilirushwa, na kuua makumi ya raia na kujeruhi mamia zaidi. Fuata matangazo kamili ya mikutano hapa chini na watumiaji wa programu ya UN News wanaweza kufuata hapa.
Fuata mipasho yetu ya moja kwa moja kutoka UNWebTV hapa chini:
© Habari za UN (2026) — Haki Zote Zimehifadhiwa. Chanzo asili: UN News