WAZIRI WA ELIMU AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WATEULE

****

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda  leo Aprili 14, 2026 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wateule watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali walizopangiwa.

Katika kikao hicho  wamekubalina kuwa  elimu, sayansi na teknolojia zitakuwa moja ya agenda za kufanyia kazi ikiwemo suala la umataifishaji elimu.

Mabalozi wateule wameipongeza Wizara  kwa mageuzi makubwa ya elimu yanayoendelea kutekelezwa na  kuahidi  kuichukua agenda ya elimu kuwa ya kimkakati kwa maendeleo ya taifa.

Mabalozi hao ni watakaoiwakilisha Tanzania  Saudi Arabia, Zambia, Muscat

 Comoros, Korea Kusini, Sweden na Umoja wa Mataifa, New York wakiongozwa na Mhe. Balozi Mhandisi Zena Said

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara hiyo.