MTATIRO AJITOSA KUWANIA UBUNGE BUNGE AFRIKA MASHARIKI

Na Mwandishi Wetu

WAKATI Chama Cha Mapinduzi  (CCM) kikifungua dirisha  kwa makada wake kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki leo,Kada wa Chama

hicho ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga amechukua fomu kuwania nafasi hiyo.

Mtatiro ambaye ni miongoni mwa makada vijana na wasomi katika Taifa la Tanzania amechukua fomu hiyo ya kuwania Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki leo Aprili 18,2026  katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, zilizopo Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Amekabidhiwa na fomu hiyo  na Ofisa wa Chama Idara ya Organaizesheni, Raymond Mosi.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu Mtatiro amesema  ameamua kujitosa katika kinyang’anyiro hicho kutumia  haki  yake ya msingi katika kuliwakilisha taifa katika Bunge la Afrika Mashariki kwa maslahi mapana ya taifa.