Natalie Portman Aibua Gumzo Baada ya Kutangaza Ujauzito wa Tatu

Global Publishers
April 18, 2026
0 Comments

Mwigizaji maarufu Natalie Portman

Mwigizaji maarufu Natalie Portman amesema anajisikia mwenye bahati na shukrani kubwa anapotarajia kumpata mtoto wake wa tatu pamoja na mpenzi wake, Tanguy Destable.

Katika mahojiano maalum, Portman alisema yeye na Destable wanafurahia sana habari hiyo. Alieleza kuwa anaona ujauzito huu kama baraka kubwa na muujiza, huku akisisitiza kuwa anafahamu changamoto ambazo watu wengi hukutana nazo katika safari ya kupata mtoto.

Portman, ambaye ana umri wa miaka 44, alisema malezi aliyopata kutoka kwa baba yake ambaye ni daktari wa uzazi yamemfanya awe na uelewa mkubwa kuhusu ugumu wa kupata ujauzito. Hivyo, anajitahidi kuwa na heshima na uelewa kwa wale wanaopitia changamoto hizo.

Natalie Portman akiwa na mpenzi wake wa zamani Benjamin Millepied

Hii itakuwa ni mtoto wake wa kwanza na Destable. Tayari ana watoto wawili Aleph mwenye umri wa miaka 14 na Amalia mwenye miaka 9 aliowapata katika ndoa yake ya zamani na Benjamin Millepied.

Amesema kuwa ujauzito huu unamfanya ajisikie tofauti ukilinganisha na ule wa awali, akisisitiza kuwa sasa ana utulivu zaidi na uelewa wa kina kuhusu maisha na watu anaotaka kuwa nao karibu. Pia anaamini huenda huu ukawa ujauzito wake wa mwisho, jambo linalomfanya kuthamini kila wakati.

Kwa upande wa afya, Portman anasema anajisikia vizuri na ana nguvu kuliko alivyotarajia. Anaendelea kufanya mazoezi mepesi kama kuogelea na mazoezi ya mwili ili kubaki imara.

Mbali na maisha ya familia, Portman pia anaendelea na kazi zake za sanaa, akiwa na miradi kadhaa iliyokamilika inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Kwa sasa, anafurahia maisha ya utulivu jijini Paris, akitumia muda mwingi kutembea bustanini, kuona sanaa, na kuwa karibu na familia yake.