Mikoa hii ijiandae kwa mvua usiku huu 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua na ngurumo kuanzia leo Jumapili Aprili 19,2026 usiku katika mikoa mbalimbali nchini.

Mikoa hiyo ni kutoka visiwa vya Unguja na Pemba, Tanga na Dar es Salaam, kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Manyara na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia).

Mikoa mingine ni ya Mtwara na Lindi, kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Katavi na Tabora, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu, Dodoma na Singida.

Pia mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe 

Kwa kesho Jumatatu, Aprili 20, 2026, imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Siku ya Jumanne ya Aprili 21, 2026 TMA haikutoa angalizo lolote la hali ya hewa lakini Aprili 22, kutakuwa na mvua kubwa mkoa wa Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

Pia Aprili 23, 2026 hakutakuwa na tahadhari yeyote juu ya hali ya hewa kulingana na ratiba iliyotolewa na TMA leo Jumapili, Aprili 19, 2026.