Amani Golugwa: Mazungumzo Yawe ya Kweli na Yenye Tija – Video

Global Publishers
April 21, 2026
0 Comments

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa, amesema chama hicho kinaamini katika mazungumzo kama njia muhimu ya kutafuta suluhu ya masuala ya kitaifa, lakini amesisitiza kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kuwa ya kweli na yenye kuleta matokeo chanya.

Akizungumza katika kipindi cha FrontPage, Golugwa alieleza kuwa CHADEMA haipingi mazungumzo wala kuyaogopa, bali inasisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya dhati yatakayojenga umoja na kuimarisha upatanishi miongoni mwa Watanzania.

Aliongeza kuwa kwa sasa taifa linahitaji majadiliano yenye tija yatakayoweka mbele maslahi ya wananchi na kusaidia kujenga mustakabali bora wa nchi.

Kwa mujibu wa Golugwa, mazungumzo yasiyo na uhalisia au nia ya kweli hayawezi kuleta mabadiliko, hivyo ni muhimu kwa pande zote zinazohusika kuwa na dhamira ya dhati ili kufikia maridhiano ya kudumu.