Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi asilia, Dkt. James Mataragio,akisisitiza jambo kwa watumishi wa EWURA alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
…..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi asilia, Dkt. James Mataragio, amewaomba waheshimiwa wabunge na wadau mbalimbali kuendelea kutembelea maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, ili kupata elimu juu ya shughuli za kimkakati zinazotekelezwa na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo pamoja na kubaini fursa za uwekezaji zinazopatikana.
Akiwa akiwa katika banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. Mataragio amesema mamlaka hiyo imeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuhakikisha uwiano kati ya maslahi ya watoa huduma na watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa, ikiwemo mafuta, gesi asilia na umeme.
“Tumeshuhudia jitihada kubwa zinazofanywa na EWURA katika kusimamia ubora wa huduma na bei stahiki, jambo ambalo linachangia kukuza uchumi na kulinda wananchi,” amesema Dkt. Mataragio.
Ameongeza kuwa uwepo wa EWURA katika maonesho hayo unatoa fursa kwa wananchi kupata elimu kuhusu haki na wajibu wao katika matumizi ya nishati, sambamba na kuelewa mifumo ya udhibiti inayolenga kuboresha huduma na fursa mbalimbali za uwekezaji.
Kwa upande wao, baadhi ya wabunge waliotembelea banda hilo pia waliipongeza EWURA kwa uwajibikaji wake, wakisema imekuwa mstari wa mbele kusikiliza na kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi katika sekta ya nishati pamoja na kuhakilisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Wiki ya Nishati 2026 imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya nishati, zikiwemo taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati kwa lengo la kuonesha maendeleo na fursa zilizopo katika sekta hiyo muhimu kwa ustawi wa uchumi wa taifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi asilia, Dkt. James Mataragio,akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw.Wilfred Mwakalosi,alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi asilia, Dkt. James Mataragio,akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw.Wilfred Mwakalosi,alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi asilia, Dkt. James Mataragio,akisisitiza jambo kwa watumishi wa EWURA alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la EWURA kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw.Wilfred Mwakalosi, mara baada ya kutembelea Banda la EWURA kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

Wabunge mbalimbali wakipata elimu walipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi asilia, Dkt. James Mataragio,akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati katika maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.